Highlights

Mshukiwa wa uhalifu aliyekamatwa jana Jumanne kuzuiliwa siku 14 kwa uchunguzi zaidi

Mshukiwa wa uhalifu wa wizi wa mifugo aliyekamatwa hapo jana Jumatatu katika kaunti ndogo ya Marsabit Central atazuiliwa kwa siku 14.

Uamuzi huo umetolewa na mahakama ya Marsabit baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la kupewa muda zaidi ili kukamilisha uchunguzi unaoendelea.

Wakili wa mshukiwa alipinga ombi hilo ila mahakama iliridhia ombi la upande wa mashtaka.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 11 mwezi ujao wa Mei.

Kulingana na idara ya polisi mshukiwa anashukiwa kuhusika katika misururu ya uhalifu wa wizi wa mifugo.

Idara ya polisi nchini imesisitiza kuwa itaendelea kulinda usalama wa raia na kuonya kuwa wote wanaojihusisha na uhalifu watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Post Comment