Highlights

Jamii ya El-Molo yapokea mashua tatu kuboresha usafiri

Na JB Nateleng

Usafiri katika vijiji vya Layeni na Komote katika wadi ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit, umerahisishwa baada ya wakaazi katika vijiji hivyo kupata msaada wa mashua tatu.

Mashua hizo zilizotolewa na shirika la Kivulini Trust, zinatarajiwa kuboresha maisha ya wakaazi ambao wameathirika na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha ziwa Turkana kuongezeka kina na kuvuruga makazi.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu Dkt. Christiana Saiti Louwa ambaye ni mwanaharakati na mtetezi wa jamii ya El Molo kupitia El Molo Forum inayoshirikiana na Kivulini Trust, amesema kuwa mashua hizo zitarahisisha usafiri wa wanafunzi pamoja na wagonjwa kuelekea nchi kavu, hatua itakayotoa afueni kwa wakazi ambao wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa za usafiri.

Aidha, ametoa wito kwa serikali kuu, serikali ya kaunti pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kuongeza mashua zaidi au kununua gari ili kuboresha huduma za usafiri kwa jamii hiyo.

Post Comment