Featured Stories / News

SHUGHULI ZA KAWAIDA ZIMEREJEA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MARSABIT BAADA YA MAAFISA WA KLINIKI KUREJEA KAZINI.  

 Na Isaac Waihenya & Ali Ibrahim Shughuli za kawaida zimerejea katika hospitali ya rufaa ya Marsabit baada ya maafisa wa kliniki kurejea kazini. Baadhi ya wananchi waliozungumza na Radio Jangwani wameeleza kwamba kwa sasa hali imeimarika na wamapata huduma za afya kama inavyaostahili. Wametaja kurejea kwa maafisa hao kama afueni[Read More…]

MAAFISA WAKLINIKI KAUNTI YA MARSABIT WAREJEA KAZINI BAADA YA KUTIA SAINI MAKUBAILIANO YA KURUDI KAZI NA IDARA YA AFYA.

Na Isaac Waihenya & Ali Ibrahim  Maafisa wakliniki katika kaunti ya Marsabit wamerejea kazini baada ya kutia saini makubailiano ya kurudi kazi na idara ya afya. Kwa mujibu wa katibu wa muungano wa maafisa wa kliniki katika kaunti ya Marsabit Abdi Shukri ni kuwa maafisa hao wa kliniki wamesitisha mgomo[Read More…]

ULIMWENGU WAADHIMISHA SIKU YA MAAFISA WA SHIRIKA LA WANYAMAPORI: WITO UKITOLEWA KWA KUWEPO KWA USHIRIKIANO MWEMA KATI YA MAAFISA HAO NA WANANCHI WA MARSABIT.

Na Isaac Waihenya & Ali Ibrahim Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya maafisa wa shirika la wanyamapori hii leo, wito umezidi kutolewa wa kuwepo kwa ushirikiano mwema kati ya maafisa hao na wananchi. Kwa mujibu wa naibu mkurugenzi wa hifadhi ya wanyamapori katika kaunti ya Marsabit Collins Omondi ni kuwa ushirikiano[Read More…]

IDADI YA DHULMA ZA KINJISIA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT VINAZIDI KUONGEZEKA MARADUFU HAYA YAKI CHANGIWA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

NA GRACE GUMATO Idadi ya dhulma za kinjisia katika kaunti ya Marsabit Vinazidi kuongezeka maradufu haya yaki changiwa na mabadiliko ya tabia nchi. Idadi hiyo katika mwaka iliyopita ilikuwa visa 14 ilhali ya mwaka huu kutoka Januari hadi mwezi uliopita ilikuwa ni visa 19 huku kaunti ndogo ya Laisamis ikiongoza[Read More…]

WATU WAWILI KATI YA ISHIRINI KAUNTI YA ISIOLO WAPO KWENYE HATARI YA KUHUSISHWA KWENYE BIASHARA HARAMU YA ULANGUZI WA BINADAMU.

Watu wawili kati ya 20 kaunti ya Isiolo wapo kwenye hatari ya kuhusishwa kwenye biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu. Haya ni kwa mujibu wa Titi Martin ambaye ni afisa wa programu ya Simba inayotekelezwa na kanisa la Salvation Army. Martin aliweka haya wazi wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya[Read More…]

MWANAUME MOJA AMESHTAKIWA KATIKA MAHAKAMA YA MARSABIT KWA KOSA LA WIZI WA MIFUGO TAKRIBAN 213.

NA CAROL WAFORO Mwanaume moja ameshtakiwa katika mahakama ya marsabit kwa kosa la wizi wa mifugo takriban 213. Inadaiwa kuwa mnamo tarehe 18 Juni mwaka 2024 katika lokesheni ya badassa kaunti ndogo ya Marsabit ya kati, kwa ushirikiano na watu wengine waliojihamu kwa bunduki mshukiwa George Leado almaarufu Lemurdato walitekeleza[Read More…]

MTU MMOJA AMETHIBITISHWA KUFARIKI DUNIA KATIKA MGODI WA HILLO ULIOKO ENEO LA DABEL ENEOBUNGE LA MOYALE.

NA CAROL WAFORO Mtu mmoja amethibitishwa kufariki dunia katika mgodi wa Hillo ulioko eneo la Dabel eneobunge la Moyale. Akithibitisha kisa hicho afisa wa upelelelezi kaunti ya Marsabit Luka Tumbo amedokeza kuwa maafisa wa polisi waliwafurusha wachimba migodi kutoka machimbo hayo mapema Jumanne asubuhi. Katika harakati hiyo watu 34 raia wa[Read More…]

Subscribe to eNewsletter