Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya ugonjwa wa kisukari siku ya Alhamisi wanadada katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kujiepusha na matumizi ya dawa za kunenepesha mili ikitajwa kuchangia ugonjwa huo.
Akizungumza na shajara ya radio Jangwani afisini mwake afisa anayesimamia ugonjwa usiokuwa wa kuambukiza Sororo Abudho amedokezo kuwa dawa hizo zina chembechembe zinazosababisha ugonjwa huo.
Sororo amedokeza kuwa visa vya ugonjwa huo vimeongezeka haswa aina ya kwanza inayopatikana miongoni mwa watoto.
Aidha amesema kuwa ugonjwa huu unachangia katika matatizo ya mbalimbali ya afya ikiwemo matatizo ya figo.
Kulingana na Sororo mtindo wa kisasa wa maisha ndio umechangia katika ongezeko la visa hivi.
Kulingana naye mtu anaweza kujizuia ugonjwa wa kisukari kwa kubadili mtindo wa maisha.
Idara ya afya jimboni itaandaa maadhimisho ya ugonjwa wa kisukari hapo kesho kwa ushirikiano na hospitali ya Havana pamoja na muungano wa Marsabit walk movement.
Hiyo kesho wakaazi watapata fursa ya kushiriki matembezi kuanzia hospitali ya rufaa ya Marsabit na kuzunguka mjini Marsabit.
Roba Godana ambaye ni mwanachama wa Marsabit Walk Movement amewataka wakaazi jimboni kujitokeza kwa wingi kwa matembezi hayo siku ya hapo kesho kwani baadhi ya magonjwa yanatokana na ukosefu wa kufanya mazoezi.
Wakaazi pia watapata nafasi ya kupata vipimo vya ugonjwa huu bila malipo pale karibu na eneo la kenya lodge.