HAMASISHO DUNI KUHUSU BIMA YA SHA NDIO SABABU KUU YA WATU KUTOJISAJILI KWA WINGI KAUNTI YA MARSABIT.
December 3, 2024
Na Isaac Waihenya & Ali Ibrahim
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya maafisa wa shirika la wanyamapori hii leo, wito umezidi kutolewa wa kuwepo kwa ushirikiano mwema kati ya maafisa hao na wananchi.
Kwa mujibu wa naibu mkurugenzi wa hifadhi ya wanyamapori katika kaunti ya Marsabit Collins Omondi ni kuwa ushirikiano mwema kati ya jamii na maafisa wa wanayamapori utahakikisha kwamba idadi ya visa vya mzozo kati ya wananchi na wanyamapori vitapungua.
Akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya sherehe hizo hapa jimboni Marsabit Omondi amedokeza kuwa ushirikiano pekee ndio utakaohakikisha kwamba hatua zinapigwa katika hifadhi za Marsabit.
Kuhusiana na usalama wa mafisaa hao Omondi ametaja kuwa shirika hilo limepoteza takriban maafisaa wawili katika mbuga ya wanyama ya Sibiloi waliouwawa na majangili wakiwa katika shughuli zao za kila siku.
Aidha, kaimu mkurugenzi wa fedha katika shirika la kuhifadhi wanyama pori nchi KWS Peter Mathenge, amewasifia maafisa hao na kuwashukuru kwa kazi njema wanayoifanya akisema kuwa shirika linatia maanani changamoto wanazokabiliana nazo maafisa katika juhudi zao za kuhifadhi mazingira na kuwalinda wanyamapori.
Kwa upande wake afisa mkuu katika idara ya maliasili na wanyama pori, kaunti ya Marsabit Bi. Pauline Marleni amesema kuwa serikali ya kaunti itaendelea kushrikiana kwa ukaribu na shirika la KWS na mashirika mengine katika azma ya utuuzaji wa mazingira, maliasili na wanyamapori hapa jimboni.