National News

Wazazi na walezi ndio wenye jukumu la kulipia chakula cha wanafunzi katika shule za msingi na upili- waziri Machogu

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu. PICHA | KWA HISANI

Na Adano Sharamo

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu amesema wazazi na walezi ndio wenye jukumu la kulipia chakula cha wanafunzi katika shule za msingi na upili.

Akihojiwa bungeni Machogu alisema hakuna sheria inayoishurutisha serikali kupitia wizara ya elimu kuwalipia wanafunzi katika shule ya msingi na ile ya upili ngazi ya chini-Junior secondary chakula cha mchana.

Aidha alisema suala la wanafunzi kulipia chakula shuleni si takwa la lazima na hakuna mwanafunzi amewai kutumwa nyumbani kwa kushindwa kulipia chakula.

Mbunge wa Teso kusini Mary Emase alikuwa amemuuliza Machogu mikakati ambayo wizara yake imeweka kuhakikisha kuwa wanafunzi kutoka familia zenye mapato ya chini hawakosi masomo kwa kukosa pesa ya kulipia chakula.

Subscribe to eNewsletter