National News

Huenda Wakenya Wanakula Vyakula Vyenye Sumu-Ripoti

PICHA: KWA HISANI

Na Adano Sharamo

Huenda wakenya wanakula vyakula vyenye sumu.

Ripoti ambayo imetolewa na shirika la Heinrich Boll Foundation inaonyesha kwamba nusu ya dawa zinazotumika na wakenya kunyunyizia mimea yao imepigwa marufuku kwenye muungano wa mataifa ya Uropa-EU kutokana na kiwango kikubwa cha kemikali.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo wakenya wanakula vyakula vyenye kemikali hatari kutokana na dawa zinazoagizwa kutoka uropa na uchina.

Washikadau katika sekta ya kilimo sasa wameitaka serikali kupiga marufuku dawa hizo kutokana na madhara ambazo zimesababisha kwa afya afya ya binadamu.

Subscribe to eNewsletter