National News

Sheria ya fedha 2023 Ilikosa Kuafikia Vigezo Kabla ya Kutekelezwa-LSK

Rais wa LSK Eric Theuri |PICHA: KWA HISANI

Na Adano Sharamo

Chama cha wanasheria nchini-LSK kimesisitiza kwamba sheria ya fedha 2023 ilikosa kuafikia vigezo vinavyotakikana kabla ya kuanza kutekelezwa.

LSK kupitia rais wa  chama hicho Eric Theuri kiliambia mahakama kuu kwamba kina wasiwasi kwamba kuna baadhi ya vipengele kwenye sheria ambavyo vina utata ikisitiza haja ya mahakama kuvifutilia mbali.

Kiliambia mahakama kuu kuhusu matozo ya asilimia 1.5 ya kodi ya kufanikisha ujenzi wa makazi ya bei nafuu.

LSK iliibua suala la kukosekana kwa sheria mahsusi inayoongoza mpango mzima.

LSK vile vile ilitilia shaka notisi iliyoipa mamlaka ya ukusanyaji kodi-KRA jukumu la kufanikisha matozo kodi ya kufanikisha mradi wa makazi ya bei nafuu.

Kadhalika LSK ilisisitiza kwamba kwa mujibu wa sheria serikali za kaunti ndizo zimetwikwa jukumu la kufanikisha masuala ya makazi.

 

Subscribe to eNewsletter