National News

Viongozi wa Azimio Wamtaka Jaji Mkuu Martha Koome Kutatua Mzozo wa Kumuondoa Mbunge Maalum Sabina Chege

Wabunge wa Azimio kwenye kikao na wanahabari PICHA: KWA HISANI

Na Adano Sharamo

Viongozi wa Azimio sasa wanamtaka jaji mkuu Martha Koome kuingilia kati na kutatua mzozo wa kumuondoa mbunge maalum Sabina Chege kwenye wadhifa wa naibu wa kiranja wa wachache katika bunge la kitaifa.

Azimio iliafikia uamuzi huo baada ya mpango wa kumuondoa Chege kupingwa na spika wa bunge hilo Moses Wetangula.

Kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa Opiyo Wandayi alikashifu Wetangula akisema kwamba anapendelea upande wa wengi katika bunge hilo kwa kufanya maamuzi wake kwa njia isiyofaa.

Azimio wanataka kumuondoa Chege na nafasi yake kuchukuliwa na mbunge wa Embakasi Magharibi David Mwenje kwa madai ya kusaliti muungano huo kwa kushirikiana na serikali ya Kenya Kwanza.

Subscribe to eNewsletter