WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Samuel Kosgei
Rais William Ruto amesema kuwa serikali itamzawidi mwanariadha Faith Kipyegon, ambaye ana rekodi ya mita 1500M na 5000M duniani, kitita cha Ksh. 5 milioni kwa rekodi moja na nyumba yenye thamani ya Ksh. 6 milioni kwa rekodi nyingine.
Akizungumza katika Ikulu ambapo alimkaribisha bingwa huyo, Rais Ruto alisema ni wakati muafaka kwa Kenya kuanza kutambua wanamichezo wake waliofanya vizuri na kuwaheshimu kwa njia inayofaa ili kuendelea kukuza ufanisi wao katika mashindano ya kimataifa.
Faith akizungumza kwenye hafla ya kuwapokea wanariadha wa kenya katika ikulu ya rais amesema kuwa hakutarajia kuandikisha rekodi hiyo mpya kwenya mbio za mita 5000 nchini ufaransa.
Kipyegon aliweka rekodi mbili za dunia katika kipindi cha wiki moja kwenye Diamond League huko Florence, Italia, na Paris, Ufaransa.