National News

Maradhi yasiyoambukiza (NCD) yasababisha vifo zaidi nchini Kenya

PICHA: KWA HISANI

Na Samuel Kosgei

Wataalamu wa afya wametoa onyo kwamba maradhi yasiyoambukiza (NCD) yanazidi kuwa tishio na kuwa sababu ya pili inayoongoza kwa vifo nchini.

Mkutano uliowakutanisha wataalamu wa afya kutoka Kaunti ya Siaya kujadili athari za maradhi yasiyoambukiza katika kaunti hiyo, ulieleza kuwa asilimia 50 ya wagonjwa katika vituo vya afya vya umma katika kaunti hiyo wanakabiliwa na maradhi yasiyokuwa ya kuambukiza.

Kulingana na mratibu wa NCDs huko Siaya, Peter Omoth, maradhi hayo yanachangia kwa pamoja asilimia 39 ya vifo katika Siaya, kiwango ambacho kinatarajiwa kuongezeka hadi asilimia 47 iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Alisema serikali ya kaunti ya Siaya imeungana na Jumuiya ya Maradhi yasiyoambukiza ya Kenya kupitia mradi wa Moyo Afya ili kuanzisha utambuzi wa mapema wa NCDs katika vituo vitano vya afya katika eneo hilo.

Subscribe to eNewsletter