National News

Kenya Kuingiza Bidhaa Bila Kodi Soko la Bara Ulaya Katika Ushirikiano Mpya na EU

Waziri wa Biashara Moses Kuria akitia saini makubaliano ya kibishara na Mwakilishi Mkuu wa EU Valdis Dombrovskis katika Ikulu ya Nairobi, Juni 19 2023

Na Adano Sharamo

Kenya imesaini mkataba wa maelewano na muungano wa bara Ulaya-EU ambao utaimarisha biashara baina ya Kenya na nchi 27 za bara Ulaya.

Akizungumza kwenye ikulu rais William Ruto amesema kwamba kwenye makubaliano hayo Kenya itaongeza kiwango cha bidhaa za kilimo ambazo zinauzwa katika masoko ya Ulaya.

Rais Ruto aidha amesema kwamba kwenye mpango huo Kenya itashirikiana na kampuni za kuzalisha bidhaa za kilimo kwenye mataifa ya bara ulaya, kuongeza thamani ya mazao hayo ya wakulima wa humu nchi.

Amesema kwamba mpango huo utaimarisha sekta ya kilimo na kuongeza nafasi za ajira.

Rais amesisitiza kwamba Kenya itaendelea kushirikiana na EU kuimarisha biashara na kufanikisha ajenda mbalimba.

Subscribe to eNewsletter