WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Samuel Kosgei
Baraza Kuu la Waislamu Kenya SUPKEM limeendelea kusisitiza kwamba serikali isijihusishe na taasisi za kidini ikizingatia kuwa Kenya ni nchi ya kidemokrasia.
Badala yake, SUPKEM imependekeza kuundwa kwa makosa ya kidini ambayo yatatumiwa kutambua watu wanaokwenda kinyume na mafundisho na ambao watakabiliwa na adhabu kulingana na sheria zilizopo.
Baraza hilo chini ya uongozi wake mwenyekiti Hasaan Ole Naado, wakati wa kutoa maoni yao mbele ya kamati ya adhoc ya Seneti kuhusu vifo vya Shakahola, pia lilipendekeza kuundwa kwa vikundi vya kidini na serikali kufanya kazi pamoja ili kufuatilia na kubainisha mafundisho yanayohusisha itikadi kali za kidini.
Hata hivyo, Jumuiya ya Waislamu ililaumu serikali kwa kile ilichokiita ubaguzi dhidi ya dini ya Kiislamu.
SUPKEM ilieleza kuwa sheria na sera za usalama kuhusu itikadi kali za kidini zilikuwa zikitumiwa kwa upendeleo dhidi ya Waislamu, ndio sababu iliyosababisha vyombo vya usalama kuchukua muda mrefu kugundua kikundi cha Paul Mackenzie.
Wakati wakidai uhuru wa kidini, viongozi hao walikiri umuhimu wa kuwa na utaratibu mzuri wa kufanikisha hilo.