National News

Akina mama kaunti ya Samburu watakiwa kujihusisha na kilimo cha ufugaji wa nyuki kama njia moja ya kujipatia mapato

Na Samuel Kosegi

Akina mama kutoka jamii za wafugaji kaunti ya Samburu wametakiwa kujihusisha na kilimo cha ufugaji wa nyuki ili kufanikisha biashara ya asali kama njia moja ya kujipatia mapato.

Haya yalijiri katika maonyesho ya mashirika yasiyokuwa ya serikali ya kuwahamasisha wafugaji kujihusisha na biashara mbali mbali.

Wadau wa mashrika hayo wamewataka akina mama hao kuzingatia kilimo hicho pasi na kutegemea mifugo pekee kwani mara nyingi kiangazi na wizi huathri mifugo.

Subscribe to eNewsletter