National News

Serekali ya kaunti ya Garissa yaanzisha mikakati ya kukamilisha miradi yote iliyokwama ya ujenzi wa masoko

PICHA: KWA HISANI

Na Isaac Waihenya

Serekali ya kaunti ya Garissa imeanzisha mikakati ya kukamilisha miradi yote iliyokwama ya ujenzi wa masoko kwa malengo ya kuimarima zoezi la ukusanyaji ushuru.

Akizungumza baada ya kuzuru masoko ya Mikono na Suuk Mac D, Gavana wa kaunti hiyo Nathif Jama alisema kando na mipango hiyo ya kuongeza idadi ya wafanyibisahara pia hilo litapunguzuza msongamano katikati mwa mji huo na pia kuogeza mapato ya kaunti.

Aidha Gavana Jama alisema kuwa fedha zaidi zimetegwa kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2023/2024 ili kujenga masoko zaidi kwenye vituo vya  biashara katika kaunti hiyo.

Subscribe to eNewsletter