Local Bulletins

WAHUDUMU WA AFYA KAUNTI YA MARSABIT WALIOHUDUMU BILA MALIPO ENZI YA CORONA WALALAMA KUTOAJIRIWA NA SERIKALI YA KAUNTI.

 

Na Lelo Wako

Vijana waliojitolea kutoa huduma hospitalini katika kaunti ya Marsabit miaka sita iliyopita wameonesha masikitiko yao ya kutoajiriwa na serikali ya kaunti hata licha ya wao kutoa huduma za afya bila mshahara kutoka mwaka wa 2018.

Vijana hao wakizungumza mjini Marsabit wameonesha masikitiko yao huku wakieleza kuwa vijana zaidi ya hamsini wamekuwa wakitoa hudumu wakati ambapo kulikuwa na janga la Corona na hata wengine wao kuambukizwa ugonjwa huo wakitoa huduma na hatimaye hawakuajiriwa.

Wameeleza jinsi walivyokuwa wakitoa huduma hospitalini wakati ambapo kulikua na vita baina ya baadhi ya jamii za Marsabit, tukio lililohatarisha maisha yao.

Vile vile wamedai kuwa wahudumu wa afya kutoka kaunti jirani na sehemu nyingine wameajiriwa badala yao.

Wamedai kuwa huenda wanaojiriwa wanatumia mbinu za kifisadi ikiwemo kutoa hongo ili kuajiriwa.

Zaidi ya hayo, wamesema kuwa  juhudi zao za kufuatilia sababu za kutoajiriwa hazijafua dafu.

Wametoa wito kwa bodi ya kuajiri wafanyakazi wa kaunti na idara ya afya kuangalia maslahi yao.

Subscribe to eNewsletter