Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
WANANCHI wa wadi ya Karare kaunti ya Marsabit wanaoishi katika maeneo yanayojulikana kisheria kuwa hifadhi za wanyama huenda wakapata afueni hivi karibuni baada ya maombi yao ya kutaka eneo hilo kuondolewa kama mbuga za wanyama kupitishwa katika bunge la kaunti ya Marsabit wiki hii.
Mwakilishi wadi wa Karare Joseph Leruk ambaye alisukuma mswada huo bungeni ameambia kituo hiki kuwa mswada huo ulipitishwa na bunge la kaunti baada ya kufuata hatua zote za kisheria.
Anasema kuwa kwa miaka mingi maeneo kadhaa ya wadi ya Karare yalisahaulika wakati maeneo mengine ya saku yalipokuwa wakiondolewa kutoka hifadhi ya wanyama. Anasema hatua hiyo ya mwanzo ni nzuri ikiashiria kuwa hivi karibuni watapata ya haki ya kumiliki ardhi yao bila hofu.
Anasema kuwa hatua iliyosalia sasa itakuwa jukumu la viongozi wa kaunti ya Marsabit kijumla kusukuma ajenda kupitishwa pia katika bunge la kitaifa. Anasema atashirikiana na mbunge wa Saku kuhakikisha bunge la kitaifa litaidhinisha ombi lao .
Amewataka wakaazi maeneo lengwa kuzidi kuwa na Imani kuwa hivi karibuni serikali itaondoa maeneo hayo kutoka kuwa hifadhi ya wanyama kwani wamesahaulika kwa miaka mingi.
Wakati uo huo ameeleza kuwa wakaazi wa eneo la Karare wataanza kuonja matunda ya kukodishwa ardhi yao kwa mwekezaji wa mkahawa wa Bongole Resort. Mkahawa huo umekodishwa kwa miaka 10 kwa mwekezaji wa kibinafsi hatua anayosema kuwa itakuza uchumi wa eneo hilo.