Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.
February 7, 2025
Baada ya kuzinduliwa kwa mfumo mbadala wa kutatua kesi nje ya mahakama hiyo jana, wakaazi katika kaunti ya Marsabit wameelezea hisia zao kuhusiana na zoezi hilo liliongozwa na jaji mkuu Martha Koome hapa Marsabit.
Baadhi ya waliozungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, wameonyesha imani yao kuwa mfumo huo ni njia mojawapo wa kurahisisha mchakato wa kuwasilisha malalamiko mahakamani na kupata haki bila kupoteza muda na rasilimali katika mchakato wa kisheria.
Aidha, wamesema kuwa wana Imani na wazee kushughulikia kesi hizo ndogo ndogo bila kupitia njia ndefu ya mahakama. Wanasema suala muhimu kwa wazee hao ni kushikilia haki na kuepuka mapendeleo.