Local Bulletins

KUNA HAJA YA KUAMINI UONGOZI WA AKINA MAMA KUTOKANA NA REKODI YAO YA UTENDAKAZI- WAKAAZI

Wakaazi wa Marsabit wametoa hisia tofauti kuhusu uwezo wa akina mama nchini kuwania urais na kushinda kiti hicho.

Miongoni mwa akina mama wanaotarajiwa kuwania urasi katika uchaguzi wa mwaka wa 2027 ni kinara wa chama cha narc kenya Martha Karua.

Wakizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee  baadhi ya wakaazi wa mji Marsabit wamesema  wakati wa akimama kushinda kiti cha urais bado haujafika ikizingatiwa bado nchi ni changa kwenye suala la demokrasia.

Aidha wengine wameshikilia kuwa mila na utamaduni ya taifa bado haiamini akinama kuweza kuongoza ikizingatiwa safari ndefu ya ukomavu wa kisiasa.

Hata hivyo baadhi ya wakaazi wamesema ya kwamba Martha Karua anatosha kuwania urais kwa sababu tangu Kenya kupata uhuru  taifa haijapiga hatua kubwa sana hivyo wangependa akina mama pia wajaribiwe.

 

Subscribe to eNewsletter