Local Bulletins

Utumizi wa dawa za kupambana na bakteria mwilini (Antibiotics) ambazo hazijaidhinishwa na mtaalamu wa afya unaweza kusababisha kifo.

Utumizi wa dawa za kupambana na bakteria mwilini (Antibiotics) ambazo hazijaidhinishwa na mtaalamu wa afya unaweza kusababisha kifo.

Kwa mujibu wa mwanafamasia katika katika hospitali ya rufaa ya Marsabitt Adan Ibro ni kuwa wakaazi wengi katika kaunti ya Marsabit wanamazoea ya kunua dawa wanapohisi maumivu mwilini jambo ambalo amesema kuwa linahatarisha maisha yao.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Adan ameelezea kuwa matumizi ya dawa hizi huenda yakafanya mgonjwa kutofika hospitali kwa wakati na kusababisha kifo.

Adan amewaonya wananchi wa Marsabit dhidi ya kusaidiana kutumia dawa pamoja akisema kuwa hatua hii itamfanya mgonjwa aliyepewa dawa hizo kukosa kutimiza dozi aliyoratibiwa na kuzui kupona maradhi anayougua kwa muda unafaa.

Kadhalika, Adan amewachangamoto wamiliki wa maduka ya kuuza dawa kutowapa watu dawa pasipokuwa na maelezo kutoka kwa mtaalamu wa afya akisema kuwa hili litasaida kupunguza visa vya matumizi mabaya ya dawa.

Subscribe to eNewsletter