Rais Ruto asikitikia hali ya usalama nchini DRC haswa ukanda wa unaokaliwa na waasi wa M23.
January 27, 2025
Wakenya wametakiwa kukataa kugombanishwa viongozi wa kisiasa na badala yake wasimame kidete kama wazalendo.
Kwa mujibu wa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Nyeri Askofu Antony Muheria kwenye ujumbe wake jana ni kuwa baadhi ya viongozi wanaeneza chuki baina ya jamii jambo linalohataisha uiano wa nchi.
Akizungumza katika ibada ya leo Askofu Muheria amewataka wananchi kutokubali kugawanyishwa na migawanyiko ya kisiasa inayoshuhudiwa nchi huku akiwataka viongozi wa kidini pia kuwa na misimamo dhabiti na kuzidi kuhubi amani.
Aidha Askofu Muheria amewataka viongozi kupima maneno yao kwa umaa kwani yanaweza kugawanya wananchi na hata kuleta uhasama.
Kiongozi huyo wa kidini ametoa wito kwa wananchi pia kutokubali kugawanywa na pia kutokubali chuki kuwagawanya na badala waishi kwa uiano na utengamano.