Gavana wa Marsabit Mohamud Ali apongeza rais Ruto kwa kuondoa hitaji la kupigwa msasa wakati wa kusaka kitambulisho….
February 6, 2025
Na Isaac Waihenya,
Serekali imejiandaa kikamilifu kuhakikisha kwamba mtaala mpya wa elimu haswa gredi ya 7,8 na 9 zinafaulu.
Haya yamewekwa wazi na mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri.
Akizungumza wakati wa halfla ya shirika la Child Fund kuzawadi wanafunzi wa shule ya msingi ya Bubisa taa za sola, Magiri amewataka wazazi kupuuza taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa kuwa idara ya elimu hajajiandaa na kutia hofu wazazi kuwa huenda JSS isifaulu, huku akizitaja taarifa hizo kama zinazopotosha.
Aidha Magiri amewataka wazazi jimboni Marsabit kuwapeleka wanao shuleni bila kuwabagua ili kubadili maisha yao ya baadae.
Magiri amesema kuwa serekali imekamilsha asilimia kubwa ya madarasa ya gredi ya 9 huku yale hayajakamilika yakitarajiwa kukamilishwa hivi karibuni.