Serikali ya kaunti ya Marsabit yakana madai ya unyakuzi wa ardhi na kutenga jamii ya Sakuye katika harakati ya kufunguliwa kwa mgodi wa Dabel.
January 13, 2025
Mwezi moja kabla ya serikali kuanza chanjo ya mifugo kote nchini, wafugaji katika kaunti ya Marsabit wametoa hisia kinzani kuhusiana na mpango huo unaolenga mifugo milioni 22.
Baadhi ya wafugaji hao wamesisitiza kuwa ni muhimu kwa serikali kuwapa maelezo ya kina kuhusu chanjo hiyo kabla ya kuanza zoezi hilo la kuchanja mifugo.
Wengine hata hivyo wamesema kuwa hawako tayari kuchanja ng’ombe wao wakidai kuwa wanahofia madhara inayoweza kupatikana kutokana chanjo hiyo.
Hata hivyo, wamewarai serikali iwasaidie kwa kuwapa msaadawa kifeda ili wafugaji waweze kuchanja mifugo yao wenyewe kulingana na magonjwa yanayowakabili.