County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

NI ASILIMIA 0.001 YA BAJETI YA KITAIFA AMBAYO HUELEKEZWA KATIKA KUSHUGHULIKIA MASWALA YA AFYA YA AKILI NCHINI. – ASEMA MTAALAM WA AFYA YA AKILI JIMBONI MARSABIT VICTOR KARANI

Na Isaac Waihenya,

 Serekali imetakiwa kuongeza mgao unaolekezwa katika kushughulia maswala ya afya ya akili nchini.

Kwa mujibu wa afisa anayesimaamia kitengo cha afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Victor Karani ni kuwa  mgao unaoelekezwa katika kushughulikia maswala ya afya ya akili ni wa chini mno.

Akizungumza hii leo wakati wa uzinduzi wa shirika la Open Mind Focus linaloshugulikia maswala ya afya ya akili hapa jimboni Marsabit, Karani amesema kuwa ni asilimia 0.001 ya bajeti ya kitaifa ambayo huelekezwa katika  kushughulikia maswala ya afya ya akili nchini.

Karani ameitaka serekali kuhakikisha kwamba inaogeza mgao huo ili kushughulikia maradhi ya afya ya akili kikamilifu kwani wananchi wengi wanaadhirika kutokana na ukosefu wa fedha za kushugulikia maradhi hayo.

Karani amezitaka serekali ya kaunti kuekeza katika afya ya akili pia kwani hamna mgao wowote ambao huelekezwa katika hilo.

Ametoa wito kwa jamii kukumbatia matibabu ya afya ya akili ili kuzuia madhara zaidi.

Subscribe to eNewsletter