Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya choo duniani, wito umetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Marasabit kuhakikisha kwamba kila boma iko na choo.
Kwa mujibu wa afisa mkuu katika idara ya afya kaunti ya Marsabit Omar Boko, ni kuwa uwepo wa vyoo katika kila boma utahakikisha kwamba jimbo la Marsabit limedumisha usafi na mazingira bora kwa wananchi.
Akizungumza kabla ya sherehe za kuadhimisha siku ya choo duniani zinazoendelea katika shule ya msingi ya msingi ya Nguruniit, Omar amesema kuwa vijiji vitatu katika eneo la hilo ambavyo ni Kilabunyo,Lekiricha na Munanda vinasherehekewa kama vijii ambao vinavyoo vya kuwamudu wananachi wote na kuzuia kutumia kinyesi ovyo yaani (Open Defecation Free).
Omar amewataka wananchi kuhakikisha kwamba wanaishi katika mazingira safi ili kujizuia dhidi ya maradhi mbalimbali yanayoweza kuipukika.
Aidha baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla ya leo wametaja kuelimishwa umuhimu wa kumiliki vyoo na kuhakikisha kwamba kila boma ina choo chake.