Local Bulletins

MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI YA SKM KAME KOTO IRAI JAMII YA MARSABIT KUWALINDA WATOTO DHIDI YA DHULMA ZA KIJINSIA.

Na Talaso Huka,

Mafunzo kuhusiana na ngono za mapema kwa wanafunzi wa shule ya msingi na ya upili ni jambo ambalo serikali ingefaa kuliangazia katika mfumo upya ya elimu.

Haya ni kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya SKM Kame Koto.

Akizungumza na Radio Jangwani afisi mwake mwalimu Koto amesema kuwa kutambulishwa kwa mafunzo haya kwa watoto kunafaa ili kuwapa wanafunzi mafunzo jinsi ya kujikinga dhidi ya mimba za utotoni.

Aidha mwalimu Kame amewahimiza wazazi kuwa mifano miema kwa wanao na vilevile kuwapa mafunzo pia kuhusiana na aadhari za matumizi za dawa za kulevya.

Vilevile mwalimu Kame ameonya walimu dhidi ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na walimu na badala yake kuwaelekeza katika njia zilizo bora.

Kadhalika mwalimu Kame amehimiza jamii kwa jumla kuwalinda watoto dhidi ya dhulma zozote za kijinsia.

Subscribe to eNewsletter