HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Isaac Waihenya,
Wahudumu wa afya wa nyajani (CHPs) pamoja na wahudumu wa afya wasaididi (CHAs) waitaja dhulma za kijinsia, mihadarati na hata ugumu wa maisha kama maswala yanayochangia ongezeko la idadi ya watu wanaougua maradhi ya afya ya akili.
Wakizungumza na vyombo vya habari wahudumu hao wa afya wakiongozwa na Daro Galgalo,Zainabu Nabosu na Jacob Kuraki wametaja kwamba jamii imekuwa ikikosa kutilia maanani maswala ya afya ya akili kutona na kuhofia unyanyapaa kutoka kwa jamii.
Wahudumu hao wa afya wameyataja hayo baada ya kuhuduria mafunzo ya siku mbili yaliyofadhiliwa na shirika la Collaborative Center for Gender and Development (CCDG) hapa mjini Marsabit na kukariri kuwa mafunzo hayo yatawafaidi katika kushughulikia maswala ya afya ya akili mashinani.