HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Caroline Waforo,
Wauguzi katika kaunti ya Marsabit wameapa kuendelea na mgomo wao hadi pale serikali ya kaunti ya Marsabit itakaposhughulikia matakwa yao yote.
Mgomo huo ambao umeingia siku yake ya nne hii leo Alhamisi umetatiza kabisa huduma za Afya katika hospitali zote za umaa hapa jimboni ikiwa ni pamoja na hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Marsabit, Hospitali ya Moyale na ile ya Laisamis.
Wauuguzi hao kupitia muungano wao wa KNUN tawi la Marsabit wamekosa kuafikiana na serekali ya kaunti ya Marsabit baada ya mkutano wa kutafuta suluhu kuandaliwa hapo jana Jumatano.
Mkutano huo uliwashirikisha washikadau mbalimbali kutoka serikali ya kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani katibu wa KNUN tawi la Marsabit Robert Matimu amesema kuwa serekali ya kaunti ya Marsabit ilikosa kutoa muda mwafaka wa kusuluhisha matakwa yao.
Wauguzi hao wanalalamikia kutolipwa mishara yao ya miezi ya Julai na Agosti.
Serikali ya kaunti ya Marsabit inadai kuchelewesha kwa mgao wake wa fedha kutoka serikali kuu.
Matimu amesema serikali ya kaunti ya Marsabit iliwataka kurejea kazini huku ikisubiri fedha kutoka bajeti ya ziada jambo na ambalo walitupilia mbali.
Itakumbukwa kuwa wahudumu wa maabara tayari walishaanza mgomo wao usiku wa kuamkia jana Jumatano huku nao maafisa kliniki kupitia muungano wao wa KUCO wakisema kuwa wataanza mgomo wao wiki ijayo.
Madaktari nao kupitia muungano wao wa KMPDU wanasubiri notisi rasmi ya kuanza mgomo.