County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News, Sport Bulletins

HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA HOSPITALI ZA UMMA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT KUZOROTEKA ZAIDI BAADA YA WAHUDUMU WA MAABARA KUANZA RASMI MGOMO WAO USIKU WA KUAMKIA LEO JUMATANO.

Na Caroline Waforo,

Huduma za matibabu katika hospitali za umma katika kaunti ya Marsabit zinataendelea kuathirika hata zaidi baada ya wahudumu wa maabara kuanza rasmi mgomo wao usiku wa kuamkia leo jumatano.

Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani kwa njia ya simu katibu wa muungano wa wahudumu wa maabara Barako Kosi ameendelea kushikilia msimamo kuwa serikali ya kaunti ya Marsabit imehujumu juhudi zao za kusajili mwavuli utakowalinda kazini mwao.

Kauli ya Barako ianjiri siku moja baada ya serikali ya kaunti ya Marsabit kupitia katibu wake Hussein Tari Sasura kukana madai hayo.

Na baada ya serikali ya kaunti ya Marsabit kusema kuwa mishara ya mwezi Julai na Agosti haijalipwa kutokana na kuchelewe kwa fedha kutoka kwa serikali kuu na hata kutoa wito kwa wahudumu wa afya kusitisha mgomo wao, wahudumu wa maabara wameikosoa serekali ya kaunti kwa kutotoa mawasiliano kwa wakati, japo wanasema kuwa wako tayari kwa mazungumzo.

Wahudumu hawa wa maabara pia wakilalama kuhusumu makato pamoja na na kutopandishwa vyeo.

Wanaungana na manesi ambao wako kwenye mgomo kwa siku tatu sasa baada ya mgomo wao kungoa nanga jumatatu tarehe 16 mwezi huu.

 

 

Subscribe to eNewsletter