Local Bulletins

UTEPETEVU WA WAZAZI WATAJWA KAMA MOJAWEPO YA MASWALA YANAYOPEKEA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI JIMBONI MARSABIT.

Na JB Nateleng,

Utepetevu wa wazazi katika kuwalea wanao umetajwa kama sababu inayochangia katika kuongezeka kwa maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Imam wa miskiti ya Jamia jimboni Marsabit Sheikh Mohamed Noor amesema kuwa, wazazi wengi wamelegeza majukumu yao ya kuwalea wanawao jambo linalochangia katika matumizi ya mihadarati na hata maambukizi mapya ya HIV jimboni.

Sheikh Noor amewataka wazazi kuwelea wanao na kuwaelekeza kwa njia bora ambazo zitawanufaisha baadae.

Sheikh Noor amewataka vijana ambao wapo kwenye mahusiano kuwa waaminifu kwa wapenzi wao na pia kufuata kanuni ambazo zitawasaidia katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Kiongozi huyo wa kidini ametoa wito kwa jamii ya Marsabit kuasi unyanyapaa kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI akisema kuwa hata wao wanafaa kushughulikiwa kama wananchi wengine jimboni.

Subscribe to eNewsletter