Local Bulletins

WASHIKADAU KATIKA SEKTA YA ELIMU WATAKIWA KUSHIRIKIANA ILI KUTAFUTA SULUHU LA KUDUMU KUHUSU VISA VYA MOTO SHULENI.

Na JB Nateleng,

Washikadau wa elimu wanafaa kuketi chini na wazazi pamoja na wakuu wa shule zote ili kuhakikisha kuwa wametoa suluhu la kudumu kuhusiana na kero la shule kuchomwa.

Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani ofisini mwake, mkurugenzi wa shirika la MWADO,Nuria Gollo ni kuwa wanafunzi wanachoma shule kusubuka kimawazo kutokana na misusrusu ya mambo katika sekta ya nchini.

Nuria amesema kuwa huenda wanafunzi wanahitaji mapumziko mafupi yaani “half-term” na ambayo huwepo katika muhula wa kwanza na wa pili jambo analotka serekali kulishughulikia ipasavyo.

Nuria amesisitiza ushirikiano kati ya wazazi, viongozi wa kidini, wakuu wa shule pamoja na idara ya elimu nchini ili kupata suluhu la kudumu kwani kwani visa hivyo vya kuteketeza shule haviadhiri tu wananfunzi bali pia vinaadhiri   wazazi.

Subscribe to eNewsletter