Local Bulletins

VIONGOZI WA KIDINI MARSABIT WASHUTUMU KISA CHA MAUAJI ELLEDIMTU MAAJUZI

Kufuatia shambulizi la Jumatatu usiku katika eneo la Elle-Dimtu eneobunge la North Horr kaunti ya Marsabit lililosababisha mauaji ya watu wanane, viongozi wa kidini jimboni Marsabit wameshtumu vikali kisa hicho huku wakitoa wito kwa idara ya usalama kufanya uchunguzi wa kina na kuwakamata waliotekeleza uhaini huo.

Sheikh Mohammed Noor ni naibu mwenyekiti wa baraza la dini mbalimbali kaunti ya Marsabit.Naye mwenyekiti wa muungano wa baraza la makanisa NCCK tawi la Marsabit Reverend Said Diba amelaani kisa hicho huku akitoa wito wa uchunguzi wa kina kufanyika.

Wahasiriwa walikuwa wanasafiri kuelekea Dukana kutumia lori ambapo walishambuliwa kwa kimiminiwa risasi kabla ya lori hilo kuteketezwa na watu waliokuwa wamevalia sare za kijeshi na kudhaniwa kutoka taifa jirani la Ethiopia.

Wakati uo huo Tume ya Uwiano na Utangamano wa kitaifa NCIC imekashifu mashambulizi hayo. Katika taarifa iliyotiwa saini na mwenyekiti wake Dr Samuel Kobia NCIC imewataka wakaazi kudumisha umoja na uwiano huku ikipongeza viongozi Jimboni Marsabit kwa kuzungumza kwa sauti moja kukemea mauaji hayo.

Subscribe to eNewsletter