Local Bulletins

SEREKALI IMEJITOLEA KUPAMBANA NA VITA DHIDI YA UTUMIZI WA MIHADARATI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT. – ASEMA DCC DAVID SARUNI.

NA ISAAC WAIHENYA

Serekali imejitolea kupambana na vita dhidi ya utumizi wa mihadarati katika kaunti ya Marsabit.

Kulingana na DCC wa Marsabit Central David Saruni ni kuwa ni swala la mihadarati ni swala linalofaa kuangaziwa kwa undani ili kuhakikisha kwamba linakomeshwe.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee,Saruni ametaja kwamba idara ya usalama inashirikiana na washikadau mbalimbali kuhakikisha kwamba wanaofanya biashara ya kuuza mihadarati mjini Marsabit haswa bangi wanatiwa mbaroni na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Ameitaka jamii kuwataja wanaoendeleza biashara ya mihadarati ili kufanikisha kukamtwa kwao.

Kuhusiana na swala la wizi wa mifugo, DCC Saruni ametaja kwamba idara ya usalama ipiga hatua kubwa katika kuhakikisha kwamba wizi wa mifugo unafikishwa kikomo.

Saruni amekariri kuwa hilo limefanishwa na doria za kila mara ambazo idara ya usalama imeimarisha katika maeneo ambayo yamekuwa yakiadhirika.

Subscribe to eNewsletter