Local Bulletins

Vijana jimboni Marsabit watakiwa kutumia vipaji vyao kukabiliana na swala la ukosefu wa ajira.

Waziri wa elimu,vijana na michezo katika kaunti ya Marsabit Bi. Ambaro Abdulahi wakati wa siku ya kimataifa ya vijana katika shule ya upili ya Moi Girls.
Picha;Radio Jangwani

 

Na Isaac Waihenya,

Wito wa vijana kutumia vipaji vyao kukabiliana na swala la ukosefu wa ajira umezidi kutotewa huku vijana wakihimizwa kukubatia ajira kidijitali.

Kwa mujibu wa waziri wa elimu katika kaunti ya Marsabit Ambaro Abdulahi ni kuwa kaunti ya Marsabit ina vipaji mbalimbali ambavyo bado havijatambuliwa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi la kushereherekea wiki ya vijana, waziri Ambaro ametaja kwamba serekali ya kaunti ya Marsabit imejitolea kuwapiga jeki vijana katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake msimamizi wa maswala ya vijana katika Shirika la CRS Irene Wairimu ni kuwa haflla hiyo ililenga kuwapa vijana fursa ya  kujikuza  na kupata maarifa ya kutatua swala ya ukosefu wa ajira.

Irene aliwataka vijana kushirikiana na mashirika mbalimbali yasiyoyakiserekali yanayowapiga jeki vijana.

Subscribe to eNewsletter