Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Silvio Nangori
Watu 25 wameaga dunia mwaka huu huku 32 wakisalia na majeraha kutokana na wizi wa mifugo kati ya wafugaji wa Kaunti za Samburu,Isiolo,Marsabit na Meru.
Akizungumza katika hafla iliyowaleta pamoja jamii mbali mbali katika hifadhi la NRT kutoka kaunti hizo, meneja wa masuala ya amani katika shirika la NRT Wario Galma amesema kuwa mifugo takriban 6,437 waliibiwa mwaka huu ila kupitia juhudi za mashirika yasiyo ya kiserikali mifugo 3,263 walirejeshwa.
Wizi wa mifugo ulioshuhudiwa mwaka huu ulitokana na visa 69 ambazo zilirekodiwa katika kaunti hizo nne.
Visa vinne vya Jaribio la wizi vilizuiliwa mwaka huu.
Kulingana na Wario mwaka wa 2023 watu 121 waliaga dunia huku 74 wakisalia na majeraha.
Wario amesema kuwa Mifugo takriban 17,050 waliibiwa na kupitia juhudi za washikadau mbali mbali Ng’ombe 10,644 walirejeshwa.
Mwaka huo visa 193 vya wizi wa mifugo vilirekodiwa idadi ya juu zaidi ikilinganishwa na mwaka huu.
Visa 11 vya jaribio la wizi wa mifugo vilizuiliwa mwaka huo.