Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Samuel Kosgei
Viongozi wa kidini bado wanarai vijana kote nchini wametakiwa kusitisha mpango wao wa maandamano uliopangiwa kufanyika Alhamisi ya tarehe 8 mwezi huu ikiwa ni shinikizo ya kumtaka rais Ruto kujiengeua mamlakani.
Viongozi hao wa kidini wakiongozwa na imam wa Msikiti wa Jamia hapa mjini Marsabit Mohammed Noor na mchungaji wa kanisa la Redeemed Gospel church silver savali wamesema kuwa tayari rais ameshasikia malalamishi ya vijana na kuna haja ya kuipa nafasi baraza jipya la mawaziri kutelekeza baadhi ya matakwa yao.
Sheik Noor akizungumza na kituo hiki asubuhi kwenye kipindi cha Amkia Jangwani amesema amesema maandamano yametosha na sasa wawe na subira.
Mhubiri Savali ameongeza kuwa ana Imani serikali imesikia malalamishi ya vijana na wananchi na hivyo kurai makundi ya vijana kusubiri serikali jumuishi ya sasa kutelekeza baadhi ahadi. Anasema maandamano yana mathara mengi yakiwemo maafa na hata uharibifu wa biashara.
Kauli yao hiyo inajiri muda mfupi baada ya baraza Kuu La Dini ya Kislamu (SUPKEM) kutoa wito kwa vijana wasitishe maandamano ambayo wanapanga kufanya Alhamisi, wiki hii na badala yake waipe serikali jumuishi nafasi ya kutimiza ahadi iliyotoa kwa raia.
Wakati uo huo amesema kuwa ameridhishwa na mapendekezo ya jopo kazi la rais lililopendekeza kudhibitiwa kwa baadhi ya wahubiri walaghai anaosema kuwa wao ndio wanaoipa jina baya wahubiri wa kikweli.
kwa upande wake Sheik Noor ameitaka mapendekezo hayo yasipite mpaka ule wa kikweli ambao wakenya wanafurahia. Hata hivyo amewataka viongozi wa kidini kufuata na kuhubiri mafunzo ya kweli.