Local Bulletins

MAAFISA WAKLINIKI KAUNTI YA MARSABIT WAREJEA KAZINI BAADA YA KUTIA SAINI MAKUBAILIANO YA KURUDI KAZI NA IDARA YA AFYA.

Na Isaac Waihenya & Ali Ibrahim

 Maafisa wakliniki katika kaunti ya Marsabit wamerejea kazini baada ya kutia saini makubailiano ya kurudi kazi na idara ya afya.

Kwa mujibu wa katibu wa muungano wa maafisa wa kliniki katika kaunti ya Marsabit Abdi Shukri ni kuwa maafisa hao wa kliniki wamesitisha mgomo wao na ambao umedumu kwa zaidi ya miezi 3, tangu tarehe 17 mwezi aprili mwaka huu baada ya serekali ya kaunti kuahidi kutatua maswala saba na ambayo waliyataka yatatuliwa kabla ya kusitisha mgomo huo.

Shukri ametaja kwamba baadhi ya maswala ambayo  serekali ya kaunti ya Marsabit imeahidi kutimiza ni ikiwemo malipo ya mshahara wa mwezi Novemba mwaka jana sawa na kuchelewshwa mishahara yao ya kila mwezi.

Shukri pia amefikichua kwamba walikubaliana kwamba kamati ya kushughulikia maswala ya kupandishwa vyeo kwa maafisa hao ibuniwe kabla ya tarehe 15 mwezi huu.

Maswala mengine na ambayo walikubaliana ni ikiwemo bima ya afya kwa maafisa hao wa kliniki pamoja na bima ya afya NHIF ambapo kulingana na Shukri walikubaliana kuhusiana na namna hilo litatekelezwa kabla ya tarehe moja mwezi Septemba mwaka huu.

Kadhalika Shukri ameweka wazi kuwa maafisa hao waklini walikubalina kwamba swala la uwakilishi lifanywe inavyafaa.

Subscribe to eNewsletter