Local Bulletins

IDADI YA DHULMA ZA KINJISIA KATIKA KAUNTI YA MARSABIT VINAZIDI KUONGEZEKA MARADUFU HAYA YAKI CHANGIWA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

NA GRACE GUMATO

Idadi ya dhulma za kinjisia katika kaunti ya Marsabit Vinazidi kuongezeka maradufu haya yaki changiwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Idadi hiyo katika mwaka iliyopita ilikuwa visa 14 ilhali ya mwaka huu kutoka Januari hadi mwezi uliopita ilikuwa ni visa 19 huku kaunti ndogo ya Laisamis ikiongoza ikufuata na Moyale kwa karibu na Saku alafu Northhorr.

Visa hivi vimekuwa nyingi katika kaunti ya ndogo ya Laisamis kwa sababu ya umaskini miongoni mwa jamii na pia imechangiwa pakubwa na mabadiliko ya tabia nchi ambayo ilisababisha mifugo nyingi kufa kutokana na kiangazi ya muda mrefu katika msimu iliyopita.

Hata hivyo visa hivyo vimetajwa kuongezeka katika kaunti ndogo ya Moyale kwa sababu maingiliano kwa mipaka kati ya Kenya na Ethiopia.

Hata hivyo wakaazi wa Marsabit wanahimizwa kuripoti visa vya dhulma vya kinjisia kwa idara inayofaa na kushauriwa pia kutonyamazia visa vya dhulma za kinjisia.

Subscribe to eNewsletter