Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Watu wawili kati ya 20 kaunti ya Isiolo wapo kwenye hatari ya kuhusishwa kwenye biashara haramu ya ulanguzi wa binadamu.
Haya ni kwa mujibu wa Titi Martin ambaye ni afisa wa programu ya Simba inayotekelezwa na kanisa la Salvation Army.
Martin aliweka haya wazi wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu kaunti ya Isiolo
Afisa huyu amedokeza kuwa wengi wa wakaazi wanahusishwa kwenye biashara hiyo kwa kisingizio cha kutafutiwa ajira humu nchini au nje ya nchi.
Ni kutokana na hilo ambapo viongozi wa kidini kaunti ya Isiolo wakiongozwa naye Ahmed sett wamewataka wananchi kaunti ya Isiolo kuwa macho ili wasiingizwe kwenye biashara hiyo.
Sett pia amewataka wale wote wanaotekeleza ulanguzi wa binadamu kukoma.
Kauli yake ikiungwa mkono na kasisi Nathan Maingi ambaye ni mwenyekiti wa INTERFAITH kunti ya Isiolo