Local Bulletins

WAZIRI WA FEDHA KAUNTI YA MARSABIT ADAN KANANO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWEZI MMOJA GEREZANI KWA KOSA LA KUDHARAU MAHAKAMA

Na Isaac Waihenya

Waziri wa fedha katika serekali ya kaunti ya Marsabit Adan Kanano amehukumiwa kifungo cha mwezi mmoja gerezani kwa kukosa kumlipa mlalamshi Petro Namweni Lochich kima cha shilingi 7,181,835 kama alivyoamrishwa na mahakama mnamo tare 15 mwezi Oktoba mwaka wa 2019.

Akitoa uamuzi huo hii leo katika MAHAKAMA ya Marsabit kupitia video hakimu mkuu Christine Wekesa ameamuru kuwa wazazri Kanano afungwe jela kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa kile alikitaja kwamba ni kudharau mahakama.

Kulingana na stakabadhi ambazo kituo hiki kimepata, Mzee Lochich aliwasilisha kesi mahakamani mnamo tarehe 8/6/2015 na kuishtaki serikali ya kaunti ya Marsabit kipindi hicho ikiongozwa na Ukur Yattani kwa unyakuzi huo wa ardhi.

Mnamo tarehe 8 mwezi huu wa julai hakimu Wekesa aliamrisha kukamatwa kwa waziri Kanano huku akimtaka kamanda wa polisi Leonard Kimayu kutekeleza jukumu hilo kutokana na serekali ya kaunti kukosa kushirikiana na mahakama katika kesi hiyo.

Subscribe to eNewsletter