Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
NA ISAAC WAIHENYA
Idara ya watoto katika kaunti ya Marsabit wazazi kuwajibika zaidi katika malezi ili kusaidia katika kupambana na utumizi wa mihadarati.
Kwa mujibu wa afisa wa watoto katika kaunti ya Marsabit Abudo Roba ni kuwa ni jukumu la kila mmoja katika jamii na haswa wazazi kuhakikisha kwamba watoto wachanga hawajiingizi katika utumizi wa mihadarati.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini mwake, Roba ametaja kwamba ni jambo la kuhuzunisha mno kuona kwamba watoto wadogo wa hadi gredi ya 3 wanavuta bangi.
Akirejelea kisa cha siku ya jumatatu wiki hii ambapo vijana watano wa kati ya umri wa miaka 9 hadi 11 katika mojawepo ya shule za msingi hapa mjini Marsabit walipatikana wakivuta bangi, Roba amewaonya wote wanaofanya biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya huku akiweka wazi kwamba yeyote atakayepatikana akiendeleza biashara hiyo atachuliwa hatua kali za kisheria.
Ameahidi kuwa watashirikiana na walimu pamoja na wazazi ili kuhakikisha kwamba watoto waliotolewa mitaani hawawafunzi wenzao utovu wa nidhamu.