Local Bulletins

IDARA YA UVUVI MARSABIT YATOA NYAVU 100 KWA WAVUVI WALIOADHIRIKA MACHAFUKO YA ZIWA TURKANA.

Na JohnBosco Nateleng

Idara ya uvuvi na kilimo jimboni Marsabit imeweza kupeana nyavu 100 kwa wavuvi walioadhirika baada ya nyavu zao kubebwa na maji ya ziwa Turkana.

Akizungumza na idhaa hii ofisini mwake Sostine Nanjali ambaye ni afisa kutoka idara ya uvuvi ameelezea kuwa wameweza kuwapa nyavu 50 wavuvi kutoka Illeret eneobunge la North Horr na nyingine 50 kwa wavuvi wa Loiyangalani, eneo bunge la Laisamis wiki iliyopita ili kuwasaida wale ambao walikuwa wamepoteza nyavu zao.

Sostine amesema kuwa watazidi kutoa nyavu hizi kwa wavuvi ili kuhakikisha kuwa wamepiga jeki suala la uvuvi Jimboni.

Sostine ameelezea kuwa kumekuwepo na ongezeko ya wamama na vijana ambao wamejitosa katika biashara ya uvuvi suala ambalo limepelekea mashirika yasiyo ya kiserekali kuingilia kati na kuwasaidia kuwapa motisha ya kuendelea zaidi kujiimarisha kiuvuvi.

Kadhalika Sostine amesema kuwa kufuatia ufadhili wa mashirika yasiyo ya kiserikali wameweza kuafikiana kuwa watakuwa wakifanya usafi wa ziwa hilo kila Jumamosi ya wiki ili kuhakikisha kuwa ziwa hilo limekuwa safi  kwa manufaa ya wenyeji na pia kuimarisha soko la samaki.

 

 

Subscribe to eNewsletter