Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
NA SILVIO NANGORI
Dhulma za kijinsia katika kaunti ya Marsabit zinazidi kuendelezwa licha ya kuwepo kwa kampeni mbali mbali za kuasi mila hizo potofu kutoka kwa mashirika za kibinafsi pamoja na serikali.
Kwa mujibu wa afisa wa jinsia katika serekali ya kaunti ya Marsabit Rose Orre ni kuwa jamii inawaficha wanaoendeleza dhulma za kijinsia kama vile ukeketaji jambo linalochochea kuongezeka kwa visa hivyo na kukosekana kwa haki kwa waadhiriwa.
Orre amesema kwamba kunyamaziwa kwa baadhi ya visa vya dhulma za kijinsia kunashusha juhudi zinazowekwa na serikali pamoja na washikadau mbali mbali jimboni.
Amesema mwaka wa 2023 ni visa 36 tu ndizo zilizoripotiwa huku idadi kubwa ya visa katika jamii zikisalia bila kuripotiwa.
Ameitaka jamii kuhakikisha kwamba waadhiriwa wa dhulma za kijinsia wanafikishwa katika hospitali ndani ya saa 72 ili kufanyiwa matibabu, ushauri na uchunguzi.