Local Bulletins

ZOEZI LA UPIMAJI WA ARDHI ILI KUWAPA HATIMILIKI WAKAAZI WA MANYATTA MADARAKA, MARSABIT LA NG’OA NANGA

Na Isaac Waihenya,

Wakaazi wa Manyatta ya Madaraka hapa mjni Marsabit wana kila sababu ya kutabasamu baada ya zoezi la upimaji wa ardhi na ili kuwapa hatimiliki za ardhi kungoa nanga.

Kwa mujibu wa MCA wa wadi ya Marsabit Central Jack Elisha aliyezungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi hilo la upimaji wa ardhi maarufu Surveying ni kuwa hatua hiyo inahakikisha kwamba wakaazi hao wamepata kumilika ardhi hiyo kikamilifu.

MCA Elisha pia amekariri kuwa wanalenga kaya zaidi ya ishirini huku hati milika za maeneo mengine kama nyayo road yalifanyw aupimaji awali zikitarajiw akwa tayari kwa muda wa miezi 6 ijayo.

Kwa upande wake afisa mkuu katika idara ya ardhi kaunti ya Marsabit Galm Guyo ni kuwa hatua ya kupata hati miliki itainua wakaazi kwa kuhakikisha kuwa wanaweza pia kupata mikopo kutumia vyeti hivyo muhimu.

Guyo vilevile amefichua kwamba serekali ya kaunti kupitia idara ya ardhi inalenga kuwapea hati miliki elfu 15 kabla ya muhula wa pili wa Gavana Mohamed Ali kukamilika.

Aidha baadhi ya wakaazi wanaonufaika na mpango huo wamepongeza serekali ya kaunti pamoja na mwakilishi wadi wao Jack Elisha kwa hatua hiyo huku wakiitaja kama itakayowainua kimaisha.

 

Subscribe to eNewsletter