Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
NA JB NATELENG
Wakazi wa kijiji cha Dikil Kimat, eneo la Loiyangalani, kaunti ya Marsabit wameamua kufanyia ukarabati barabara ambayo ilikuwa imeharibiwa na mafuriko yaliyoshuhudiwa katika eneo hilo mwezi wa nne mwaka huu.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu, Joseph Atele ambaye anaongoza shughuli hiyo amesema kuwa waliafikia hatua hii baada ya wao kupata changamoto ya kupokea huduma muhimu kwani biashara nyingi ziliweza kukadiria hasara baada ya magari na pikipiki kukosa kufika katika Kijiji hicho.
Joseph ameelezea kuwa, ilikuwa pia vigumu kuwapeleka wagonjwa pamoja na akina mama kupata matibabu kwa sababu ya ubovu wa barabara na mara nyingi huwa wanatumia barabara ndefu ambayo huwa inachukua saa nyingi kuwafikisha hospitalini.
Kadhalika Joseph ameitaka serekali kuweza kuwasaidia katika kuwatengenezea barabara hiyo kwa kujenga daraja ili kuwawezesha kufanya uchukuzi hata wakati ambapo kuna mvua kwani wanahofia kuwa huenda wakawa wamefanya kazi ya bure kwani mvua itakaponyesha katika eneo hilo, itasomba barabara hiyo na kuwafanya tena kuwa na tatizo ambalo wamekuwa wakijaribu kulitatua kwa muda.