Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
NA LELO WAKO
Waziri wa Ardhi, Ukuaji wa mji na Kawi katika kaunti ya Marsabit, Amina Chala amesema kuwa idara ya ukuaji wa mji itaweka mikakati kuweka taa za barabarani mjini Marsabit ili kuimarisha usalama na kusaidia wanabiashara kuendeleza biashara hata nyakati za usiku.
Akizungumzia hitilafu iliyo ofisini mwake waziri Amina ameeleza kuwa tatizo hilo linalokumba wakaazi kwa muda mrefu limesababishwa na hatua ya mwakandarasi (EP Global) kutokabidhi mradi huo kwa serikali mwaka wa 2017 kutokana kesi ya deni la milioni 36 inayodai kaunti tatizo analosema limerejesha nyuma mchakato huo.
Anasema wanafanya juhudi kutatua suala hilo ikiwemo kutumia njia ya mazungumzo na kuelewana na wanakandarasi huyo ili kukabidhi majukumu ya kuweka taa hizo wizara yake.
Hata hivyo Amina amesema kuwa idara yake imezindua taa kubwa za ‘Flood Lights’ katika maeneo mbalimbali ikiwemo mjini Marsabit hatua anayosema kuwa imewezesha wanabiashara mjini kufanya shughuli zao hata wakati wa usiku.
Vile vile, Amina Chala akizungumzia mipango ya usoni, ameeleza kuwa watashirikiana na mashirika mbalimbali ili waweze kuwekeza mradi wa taa za barabarani mjini katika mwaka huu.