Local Bulletins

VIONGOZI WA KIDINI KAUNTI YA ISIOLO WATAKA WANANCHI KUWASAMEHE WABUNGE WALIOPIGIA KURA MSWADA WA FEDHA 2024.

Na Samuel Kosgei,

Wito umetolewa kwa wakaazi kaunti ya Isiolo na wakenya kwa ujumla kuwasamehe na kuwapea wabunge nafasi ya kuwahudumia licha ya wao kupitisha mswada uliokuwa umepingwa na wakenya.

Wito huo umetolewa na Ahmed Sett ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa viongozi wa kidini kaunti ya Isiolo

Akihutubia wanahabari Sett amesema wabunge tayari wameonyesha nia ya kubadili miendeo yao ikiwemo kukataa nyongeza ya mshahara

Wakati uo huo amewapongeza vijana wa kizazi cha Gen Z kwa kuonyesha ukakamavu wa kupigania haki yao pamoja na uongozi bora humu nchini

Kando na hayo Ahmed Sett ambaye pia ni mweka hazina wa baraza kuu la wazee nchini amewataka wanasiasa kaunti ya Isiolo na Kenya kwa jumula kutotoa matamshi ambayo yanaweza kuligawanya taifa

 

Subscribe to eNewsletter