Local Bulletins

SHIRIKA LA LAKE TURKANA WIND POWER (LTWP) LAZINDUA KISIMA CHA MAJI KWA WAKAAZI DAKAYE-MOITE, LOIYANGALANI.

Na Ambassador Kontoma

Wakaazi wa Dakaye-Moite katika wadi ya Loiyangalani wanasababu ya kutabasamu baada shirika la Lake Turkana Wind Power(LTWP) kuwachimbia kisima cha maji. Kisima hicho kitawafaidi wakaazi takriban nyumba elfu tatu katika wadi ya Loiyangalani kwa maji Safi ya kunywa.

Katibu kutoka Idara ya Maji Rob Galma aliongoza hafla hiyo ya kisima hicho kukabidiwa kwa Jamii ya Dakaye-Moite kwa ufunguzi wa kisima hicho rasmi.

 Wakati uo huo, Katibu huyo wa serikali amepeana tenki moja ya maji ya Lita 20,000 na kuahidi kupatiwa mafunzo kwa kamati ya maji ili waweze kujua umuhimu wa kutunza maji kwa Jamii ya Dakaye-Moite na viunga vyake.

Ufunguzi wa kisima hicho itapunguza uhasama wa Jamii wanaozozana juu ya maji kwa muda mrefu huku Amani na usalama ikitabiriwa kuonekana kufuatilia kuchimwa kwa kisima hiki.

Katibu huyo pia ameshukuru na kupongeza shirika la Lake Turkana Wind Power Limited kwa utendekazi wao vyema katika Jamii. Pia amewasihi wakaazi wa Dakaye-Moite kuitunza vizuri kisima kwa njia nzuri inayotakikana.

Subscribe to eNewsletter