Local Bulletins

Serikali yatakiwa kuongeza maafisa wa NPR eneo la Badasa na Songa ili kuimarisha usalama.

 Na Samuel Kosgei

Idara ya usalama hapa Marsabit imetakiwa kuwapa maafisa wa akiba (NPR) bunduki za kulinda jamii katika maeneo ambapo ukosefu wa usalama hushudiwa mara nyinyi katika eneobunge la Saku.

MCA wa Karare Joseph Leruk akizungumza kwenye kikao kimoja cha shiriika la NRT mjini Marsabit amesema kuwa inashangaza kuona kuwa wakaazi wa maeneo ya Badasaa, Songa, Leyai na maeneo ya karibu yalikosa kutengewa maafisa Wa NPR licha ya kuwa eneo hilo ni sehemu hatari ikija ni suala la usalama.

Leruk sasa anamtaka kamishna mpya sawia na kamanda mpya wa polisi kuipa eneo hilo uzito kwenye suala la kuimarisha usalama.

Kauli yake Leruk inajiri wiki chache baada ya hali ukosefu wa usalama kushuhudiwa katika sehemu hizo za Badasa na Songa.

Leruk aidha ameitaka idara hiyo ya usalama kuhakikisha kuwa lokesheni ambazo hazina machifu kwa sasa katika wadi ya karare na kwengineko nafasi hizo zijazwe kwa haraka  ili ipige jeki suala nzima la usalama.

Kwa upande wake kamishna msaidizi wa Marsabit Central Richard Chepkong’a amesema kuwa serikali itazingatia maoni ya viongozi na kuchukua hatua kutokana na ulegevu uliopo.

Aidha Chepkonga ametahadharisha vijana wa Marsabit dhidi ya kuchoma barabara wakati wa maandamano wanayofanya kupinga serikali akisema kuwa ni vyema kulinda rasilmali za serikali kwani zinalenga kuwafaa wananchi.

Subscribe to eNewsletter