Local Bulletins

Huduma za matibabu hospitali kuu ya Marsabit zalemazwa kufutia mgomo wa wahudumu wa afya.

NA GRACE GUMATO

Huduma za hospitali ya rufaa ya Marsabit zimelemezwa  hii leo kutokana na kuandamana kwa wafanyikazi wa hospitali hiyo baaada ya kulalamika kuwa hawajalipwa mishahara ya mwezi mitatu.

Aidha wanafanyikazi hao ikiwemo madaktari na wauguzi wa hospitali hawajalipwa kwa miezi mitatu huku wafanyikazi wasio wa kudumu wakidai hawajalipwa kwa miezi saba ilhali madaktari wanafunzi wakidai kuwa hawajalipwa kwa muda wa miezi minane.

Pia wanadai kuwa makato yao ya kila mwezi yanayofaa kuwasilishwa kwa idara za serikali kama vile NHIF, NSSF hata michango wa saccos haiyafiki ofisi hizo ilhali zinakatwa kila mwezi.

Wafanyikazi hao wa hospitali wanasema kuwa mgomo huo haujafanyika kikamilifu hii leo kutoka na mgomo wa vijana wa Gen-Z unaoendelea na pia kukatazwa barua kutoka kwa afisa wa polisi ili kuruhusiwa kuandama.

Hata hivyo wameahidi kuadamana tena siku ya Jumatatu ijayo mpaka matakwa yao yatimizwe na serikali ya kaunti ya Marsabit.

Aidha hospitali ya Marsabit Alhamisi ilisalia kufungwa na shughuli ya matibabu kusitishwa.

Subscribe to eNewsletter